1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels wafikia makubaliano juu ya pkupunguza utoaji wa gesi ya Carbon dioxide.

Mohammed Abdul-Rahman9 Machi 2007

Ni kwa alau asili mia 20, ifikapo 20020 ili kupunguza janga la uharibifu wa mazingira.

https://p.dw.com/p/CHIY
Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya Angela Merkel akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na waandishi habari mjini Brussels.
Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya Angela Merkel akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na waandishi habari mjini Brussels.Picha: AP

Viongozi wa mataifa wanachama wa umoja wa ulaya, wameidhinisha mpango wa kuchukuliwa hatua zenye lengo la kuufanya umoja huo, uchukuwe uongozi duniani katika suala la kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Makubaliano hayo juu ya kuchukuliwa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani, ni pamoja na kuwekwa mkatati maalum unaohusiana na matumizi ya nishati mbadala. Kwa mujibu wa mjumbe mmoja, aliyezungumza baada ya uamuzi wa viongozi 27 wa nchi wanachama ,mkakati huo unahusiana na kupunguzwa kiwango cha utoaji wa gesi ya carbon dioxide .

Chini ya Uwenyekiti wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye nchi yake ndiyo mwenyekiti wa sasa wa umoaja huo,makubaliano hayo yanaruhusu paweko na ridhaa kwa kila nchi kujitolea jinsi itakavyochangia kufikia lengo la pamoja la umoja wa ulaya juu ya matumizi ya vyanzo mbadala kama nishati ya jua, upepo na nishati ya umeme kwa msukumo wa maji, kama sehemu ya mkakati wa kupunguza utoaji wa gesi ya carbon dioxide inayochafua mazingira, kwa asili mia alau 20 ifikapo 2020.

Kandoni mwa suala hilo la mazingira, Viongozi wa umoja wa ulaya, walizungumzia pia masuala ya siasa aza kimataiafa. Kuhusu mashariki ya kati wakaelezea kuunga mkono serikali ya umoja wa taifa aya Wapalestina inayotarajiwa kuundwa kati ya Hamas na Fatah, lakini waskishikilia kwamba serikali hiyo ya mseto haina budi kuitambua Israel. Walisema umoja wa ulaya utakua tayari kushirikiana na serikali halali ya wapalestina, itakayokubaliana na madai ya kimataifa ambayo ni kumalizwa matumizi ya nguvu na kutambuliwa dola ya Kiyahudi. Rais Jacques Chirac wa Ufaransa alisema mkataba wa Mecca ulioasainiwa na pande hizo mbili Hamas na Fatah unafungua njia ya kuelekea katika kile anachotarajia kuwa ni maelewano, amani na usalama.

Aidha kwa upande mwengine , waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair alisema amekua na mazungumzo muhimu kujaribu kuwarai viongozi wengine kutuama wanajeshi zaidi kukiimarisha kikosi cha umoja wa kujihami wa magharibi-NATO, katika mapambano dhidi ya Watalibani nchini Afghanistan. Akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano huo wa kilele, Blair alisema suala hilo ni la umuhimu mkubwa kwa usalama wa nchi za ulaya na ulimwengu kwa jumla.

Uingereza, Marekani ,Canada na mataifa mengine yalioko katika kikosi hicho cha NATO kusini mwa Afghanistan, yamevunjwa moyo na kusita kwa baadhi ya nchi shirika za ulaya katika kuchangia wanajeshi zaidi katika jeshi hilo la NATO la askari 35,500, na hasa katika kuwaruhusu wanajeshi wao kushiriki katika mapambano dhidi ya watalibani, kusini na mashariki mwa Afghanistan.