1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa wasomali umeahirishwa.

13 Aprili 2007

Mkutano uliokua uhudhuriwe na wajumbe 3000 wa koo za kisomalia kurejesha suluhu nchini umeahirishwa.

https://p.dw.com/p/CHGL

Kutokana na machafuko ya umwagaji damu na wimbi la wakimbizi nchini Somalia,mkutano wa kuleta suluhu na maskizano nchini humo uliopangwa kati ya mwezi huu sasa umeahirishwa.

Umoja wa Ulaya unahimiza mno kifanyike kikao hicho ambacho kwa jicho la serikali ya mpito ya Somalia, hadi wajumbe 3000 wa koo za kisomali wahudhurie.

Kuwa mkutano huo wa kuleta masikizano ungefanyika jumatatu hii ijayo,hakuna awali alieamini .Wajumbe 3000 wanaowakilisha koo mbali mbali za kisomali kuweza kukusanyika mjini Mogadishu hata katika hali shuar, si kazi rahisi.Na kwa jicho la vita vinavyowaka moto mnamo miaka 16 sasa,hili ni jambo lisilowezekana kabisa.

Ngumu zaidi ya mipango ya maandalio kwa mkutano huu, ni kukataa katakata kwa serikali ya mpito ya Somalia kuwaalika mkutanoni wafuasi wenye siasa ya wastani wa Mahkama za kiislamu kama vile waziri wa nje wa Ujerumani alivyodai mapema mwaka huu kwa niaba ya Umoja wa Ulaya.

Badala ya kunyosha mkono wa suluhu na kuyafikiria mahitaji ya usalama ya wananchi wanaoungamkono kwa kadiri kubwa mahkama za sheria,serikali ya mpito ya Mogadishu inawaandama wakereketwa wa haki za binadamu na vyombo huru vya habari,imemtimua spika wa Bunge na kuruhusu ndege za helikopta za mshirika wake Ethiopia kuvuma juu ya maeneo ya raia.Na nini yasema jamii ya kimataifa ?

Hukutana mara moja kwa mwezi katika lile kundi la mawasiliano na Somalia ili kuzitaka pande zinazogombana kuweka chini silaha na kukaa katika meza ya mazungumzo.

Mchezo huu wa aibu unafaa sasa kukoma kwavile orodha ya hatua barabara zinazofaa kuchukuliwa imekuwa ikiongoja kitambo sasa.

Ethiopia ambayo inaangaliwa na wasomali kuwa dola lililoikalia nchi yao na la kikristu katika ardhi ya waislamu,yafaa kushinikizwa kuondoa majeshi yake nchini Somalia.Ikiwa haitafanya hivyo karibuni, wafuasi wenye itikadi kali zaidi za kiislamu nchini Somalia, watapata nguvu katika kupaza sauti na kuwaita wasomali wenye siasa wastani kujiunga na vita vya Jihad dhidi yao.

Katika swali hili, Marekani mjini Washington, inapaswa pia kufikiri upya uungaji wake mkono wa serikali ya Ethiopia, inayotikiswa ndani na wananchi wake na inayoitumia kama polisi wake kupambana na ugaidi katika Pembe ya Afrika.

Mwishoe, yafaa kujiuliza:kwanini Somalia kila mara inarudi katika janga la machafuko ?

Sababu ni kuwa mizozo ya ndani ya Somalia na ile ya kimkoa, imefungamana pamoja.Pili, ni kwa kuwa sera ya Marekani ya kupiga vita ugaidi katika Pembe ya Afrika, haikuzingatiwa vyema sawa na vile Irak.Isitoshe, badiliko la sera kabla kumalizika kipindi cha utawala wa Bush,kusitegemewe.