1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Bomu limeua walinzi wa amani Somalia

17 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1L

Wanajeshi 4 wa Umoja wa Afrika wameuawa na 5 wengine walijeruhiwa,kaskazini mwa mji mkuu wa Somalia,Mogadishu katika mripuko wa bomu lililotegwa kando ya barabara.Vile vile mtoto mmoja aliekuwa akicheza mpira karibu na mlolongo wa magari ya vikosi vya Uganda yaliyolengwa, aliuawa katika mripuko huo.Wanajeshi wa Uganda wapatao kama 1,500 wamepelekwa Somalia kulinda amani kama sehemu ya kikosi cha wanajeshi 8,000 kinachotazamiwa kupelekwa na Umoja wa Afrika. Mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika,Alpha Omar Konare ametoa mwito wa kukomesha mashambulio ya aina hiyo.Akisifu kazi zinazotekelezwa na walinzi wa amani katika hali zilizo ngumu sana,ametoa mwito wa kuwaunga mkono wanajeshi wa Umoja wa Afrika.