1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Watu tisa wauwawa kwenye mripuko wa bomu

16 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIR

Bomu la zamani la kutegwa ardhini limeripuriwa kwa bahati mbaya na watoto na kuwaua watu tisa, wakiwemo watoto watano, hii leo mjini Afgoye karibu na mji mkuu Mogadishu nchini Somalia. Watu wanne wamejeruhiwa akiwemo mwanamke mmoja aliyepoteza mkono wake.

Duru za polisi zinasema bomu hilo lilichimbwa na watoto wa wakimbizi waliokimbilia mji wa Afgoye magharibi mwa Mogadishu kwa sababu ya machafuko. Mripuko ulitokea wakati watoto hao walipolirusha bomu hilo motoni.

Kamanda wa polisi mjini humo, Ibrahim Dini Isak, amesema mripuko huo umeziharibu kabisa nyumba mbili lakini halikuwa shambulio la kigaidi.