1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Mfanyikazi wa WFP kuendelea kuzuiliwa

19 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7ES

Afisa mmoja wa ujasusi nchini Somalia anaeleza kuwa mfanyikazi wa Mpango wa Chakula Ulimwenguni WFP aliyekamatwa wiki hii ataendelea kuzuiliwa jela mpaka uchunguzi wa uhalifu ukamilike.Kwa mujibu wa mkuu wa Idara ya ujasusi ya taifa nchini Somalia Jenerali Mohamed Warsame Darwish mfanyikazi huyo yuko salama na anatazamwa vizuri.Mafisa wa usalama walivamia afisi za Umoja wa mataifa mjini Mogadishu siku ya jumatano na kumkamata Idris Osman ambaye ni mkuu wa shirika hilo la chakula ulimwenguni WFP.

Hatua hiyo ilipelekea shirika hilo kusitisha msaada wa chakula hapo kwa papo unaolenga kusaidia yapata watu alfu 76.Kulingana na shirika hilo wameweza kuzungumza na Bwana Osman kwa simu aliyesema kuwa hana majeraha yoyote ila haijulikani iwapo alilazimishwa kusema hayo.