1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moqtada el-Sadr atishia kufanya uasi wa kijamii Iraq.

25 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DUEn

Basra.

Kiongozi wa kidini nchini Iraq Moqtada al-Sadr ametishia kufanya kampeni ya nchi nzima ya uasi wa kijamii baada ya mapigano makali kuzuka katika mji wa kusini wa Basra kati ya majeshi ya usalama ya Iraq na wanamgambo wake wa Kishia, wa jeshi la Mehdi.

Mwakilishi wa Sadr katika mji mtakatifu wa Najaf alisoma taarifa ambayo inawataka Wairaq kuchukua hatua ya kukaa chini nchi nzima.

Miito hiyo ni kutokana na operesheni inayofanywa na jeshi la Iraq ya kuchukua udhibiti kutoka kwa wanamgambo na makundi ya wapiganaji mjini Basra, mji wa pili kwa ukubwa nchini humo.

Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki yuko mjini humo akiangalia uendeshaji wa operesheni hiyo ambapo wanajeshi wapatao 50,000 wa Iraq pamoja na polisi wanashiriki.