1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MORONI:Kanali Bakary alaumiwa na Umoja wa Afrika AU

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBej

Umoja wa Afrika unamlaumu kiongozi wa kisiwa cha Nzouani huko Komoro kwa kuasababisha mkwamo mpya wa kisiasa .Kanali Mohamed Bakary alijitangaza mshindi baada ya uchaguzi wa rais kisiwani Nzouani.Uchaguzi huo ulifanyika bila idhini ya Umoja wa Afrika na serikali kuu ya Jumuiya ya Komoro.

Umoja wa Afrika inasisitiza kufanyika kwa uchaguzi ulio huru na haki kisiwani Nzouani.Visiwa vya Komoro vinajumuisha maeneo ya Moheli,Ngazija na Nzouani na kupokezana urais wa serikali kuu.Kwa mujibu wa mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika Francesco Madeira Bwana Bakary ndiye chanzo cha utata visiwani Komoro.Mjumbe huyo anafanya mazungumzo na maafisa wa serikali ya kisiwa cha Nzouani na serikali kuu kabla kuwasilisha matokea kwa Umoja huo.Serikali kuu inatoa wito wa msaada wa kijeshi ila mbunghe mmoja wa kisiwa hicho anasema kuwa kiko tayari kujilinda.