1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Hakuna mgogoro kati ya Urusi na Umoja wa Ulaya

16 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1R

Serikali ya Moscow imekanusha kuwa uhusiano wa Umoja wa Ulaya na Urusi unakabiliwa na mzozo. Mjumbe wa Urusi katika Umoja wa Ulaya,Sergei Yastrzhembsky aliwaambia maripota kuwa Brussels na Moscow zinajaribu kutenzua matatizo yaliopo hivi sasa.Akakubali kuwa daima,kulikuwepo matatizo,lakini hali hiyo isichukuliwe kama ni ishara ya mzozo.Matamshi yake yametolewa siku moja baada ya mkutano wa waziri wa nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier pamoja na rais wa Urusi Vladimir Putin.Steinmeier alikwenda Moscow kuzungumza masuala ya utata kama vile mustakabali wa jimbo la Kosovo,Urusi kuzuia kuagizia nyama kutoka Poland-nchi iliyo mwanachama katika Umoja wa Ulaya na suala la kuondoshwa kwa sanamu ya ukumbusho wa vita ya enzi ya Soviet Union ya zamani,nchini Estonia.