1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Putin na Larijani wajadili mradi wa kinuklia wa Iran

11 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtm

Duru za habari nchini Urussi zinasema,rais Vladimir Putin ameanza kufanya majadiliano pamoja na mpatanishi wa Iran,Ali Larijani kuhusu mgogoro wa kinuklia wa Iran.Duru ya Kremlin iliyonukuliwa na shirika la habari la Interfax imesema, majadiliano hayo yanafanywa katika nyumba ya Putin nje ya mji.Mbali na mgogoro wa kinuklia wa Iran,mazungumzo hayo,yatashughulikia pia uhusiano wa nchi hizo mbili na matatizo ya eneo hilo. Waziri wa kigeni wa Urussi,Sergei Lavrov vile vile anahudhuria mazungumzo hayo.