1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Rais wa Misri, Hosni Mubarak, yuko nchini Rushia

1 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCx2

Rais wa Misri Hosni Mubarak, amewasili mjini Moscow leo kwa ziara ya siku tatu nchini Rushia.

Rais Mubarak atakuwa na mazungumzo na rais wa Rushia, Vladimir Putin, juu ya masuala ya mauzo ya silaha na nguvu za kinyuklia. Makamu waziri wa mambo ya kigeni wa Rushia, Alexander Saltanov, ambae amempokea rais Mubarak, amesema ziara hiyo ni yenye umuhimu mkubwa ukizingatia hali ilivyo mashariki ya kati na ambayo kwa bahati mbaya imezidi kuwa mbaya. Saltanov, ameongeza kusema kwamba Misri ni mshirika wa Rushia katika eneo hilo la mashariki ya kati.