1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Russia yasitisha ushiriki wake katika mkataba wa upunguzaji silaha.

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79B

Bunge la Russia limepiga kura kwa kauli moja kusitisha ushiriki wa nchi hiyo katika mkataba muhimu wa Ulaya wa kudhibiti silaha. Bunge hilo Duma lilipiga kura kuunga mkono amri iliyotolewa na rais Vladimir Putin aliyoitoa mwezi Julai mwaka huu. Hatua hiyo inaonekana kwa kiasi kikubwa kuwa inakuja kujibu mipango ya Marekani ya kujenga mfumo wa ngao dhidi ya makombora nchini Poland na jamhuri ya Chek. Mkataba huo kuhusu majeshi ya kawaida katika bara la Ulaya ulitiwa saini na mataifa 16 wanachama wa NATO pamoja na wanachama sita wa mkataba wa zamani wa Warsaw mwaka 1990. Mkataba huo unaweka viwango maalum vya silaha zinazoruhusiwa nchi moja kuwa nazo katika eneo kuazia milima ya Ural nchini Russia hadi katika pwani ya bahari ya Atlantic ya Ulaya ya magharibi.