1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Wanaharakati wa kutetea ushoga wapigwa.

28 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxU

Watu wenye msimamo mkali wa kizalendo na waumini wenye imani kali wa kanisa la Orthodox wamewapiga mangumi na mateke waandamanaji wanaodai haki ya wasenge ambao walikuwa wakiandamana mjini Moscow.

Polisi wa Russia waliwakamata kwa muda wabunge wawili waliotembelea mji huo kutoka umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na mwanachama wa chama cha ulinzi wa mazingira cha Green kutoka bunge la Ujerumani, Volker Beck.

Kiasi cha wanaharakati 30 wa kutetea haki za wasenge wamekamatwa na polisi , baada ya kuwa wanaangalia tu wakati waandamanaji hao mjini Moscow wakishambuliwa baada ya kufanya maandamano ambayo hayakuruhusiwa.

Waandamanaji hao walikuwa wakijaribu kutoa malalamiko yao kwa meya wa mjini Moscow, wakidai haki ya kufanya maandamano hadharani.