1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Waziri wa kigeni wa Marekani ziarani Urussi

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0c

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Condoleezza Rice anaikamilisha ziara yake barani Asia kwa kuitembelea Moscow leo hii.Wakati wa ziara hiyo fupi,Bibi Rice anaonana na rais Vladimir Putin,waziri mwenzake Sergei Lavorov na waziri wa ulinzi Sergei Ivanov wa Urussi.Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Urussi,mazungumzo ya viongozi hao yatahusika na njia ya kutekeleza vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea ya Kaskazini.Hata mgogoro unaohusika na mradi wa kinuklia wa Iran utajadiliwa.Hapo awali mjini Beijing,Rice na waziri mwenzake wa China,Li walitoa mwito kwa Korea ya Kaskazini,irejee katika majadiliano yanayohusika na mgogoro wake wa kinuklia.