1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow.Olmert aiomba Urusi kushirikiana katika kuiwekea vikwazo Iran.

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1B

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ameiomba Urusi kusaidiana katika kuizuia Iran isitengeneze silaha za nyuklia.

Olmert yupo mjini Moscow kwa mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin.

Kabla ya mkutano wao, waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov alisema kwamba, anahisi hakuna haja ya kufanya chochote juu ya mradi wa kinyuklia wa Iran.

Ehud Olmert pia amesisitiza kwa Urusi kwamba vikwazo vya silaha lazima viwekwe dhidi ya Iran na Syria kutokana na kuwapelekea silaha wanamgambo wa Hezbollah walioko nchini Lebanon, ambao walipigana vita vya wiki sita na Israel mnamo majira ya kiangazi ya mwaka huu.