1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow.Sergei Lavrov audharau mswaada mpya wa Azimio la Umoja wa Mataifa.

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCz3

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amenukuliwa akisema kuwa, mswaada mpya wa azimio la Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran hauna maana yoyote katika kulishughulikia suala la mvutano wa kinyuklia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Urusi Interfax, Lavrov amesema, mapendekezo ya mwisho yameshindwa kuorodhesha malengo yatakayohakikisha kuwa Tehran haitajipatia teknolojia tete ya kinyuklia na wakati huo huo kuwacha wazi njia zote za majadiliano.

Mswaada wa mwisho uliowasilishwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi za Umoja wa Ulaya utajadiliwa baadae hii leo.