1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mripuko wa bomu Gaza waua 7

16 Februari 2008

Mwanaharakati wa Islamic Jihad na familia yake wauwawa

https://p.dw.com/p/D8Nz

GAZA

Takriban watu saba wameuwawa na wengine 40 wamejeruhiwa kufuatia mripuko wa bomu uliotokea katika nyumba ya mwanaharakati wa ngazi ya juu wa kundi la wanamgambo wa kiislamu la Islamic Jihad katika ukanda wa Gaza.Taarifa za hospitali zinasema baadhi ya watu waliojeruhiwa wako katika hali mbaya.Maafisa wa kundi la Islamic Jihad wanasema Israel ililenga shambulio hilo dhidi ya nyumba ya Ayman Atallah Fayed kwenye shambulio hilo la angani lakini polisi wa Hamas wanadai chanzo cha mripuko huo hakijulikani.Fayed anasemekana kuwa miongoni mwa watu waliouwawa pamoja na watu wa familia yake.