1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muandishi habari wa kijerumani huru ?

25 Julai 2007

Kuna taarifa kuwa muandishi habari wa kijerumani alietekwanyara jana usiku huko Afghanistan sasa ni huru.Habusu 1 wa Korea kusini asemekana ameuwawa.

https://p.dw.com/p/CHk1

Watekanyara wa kitaliban wamemua mateka wao wa kwanza kati ya wakorea kusini 23 waliowatia nguvuni na wametishia kuwaua wengine ikiwa madai yao hayakuitikiwa.Kuna taarifa kutoka Seoul, kuwa wakorea kusini 8 kati ya hao wamekombolewa leo na wamehamishiwa mahala pa usalama.

Hatima ya muandishi habari wa kijerumani aliesemekana ametekwanyara mapema hii leo bado haijulikani wazi ingaswa kumekua na tetesi kuwa ameachiwa.

Kwanza ulikua uvumi ambao ulizagaa mjini Kabul,lakini baadae sio tu idara ya usalama ya Afghanistan imethibitisha bali hata duru za usalama za kambi ya magharibi.

Hata gavana wa jimbo la Kunar amethibitisha kutekwa nyara kwa muandishi huyo.Msemaji wake amesema ujumbe wa watu 5 wa gavana ulifika katika kijiji cha Sangar kwenye wilaya ya Watapur na huko ukathibitisha kuwa ripota huyo wa kijerumani alinyakuliwa jana usiku huko pamoja na waafghani 2 waliofuatana nae.

Wazee wa kijiji hicho pamoja na wakuu wa serikali wanajaribu kumkomboa.Eneo hilo karibuni hivi lilikua mahala pa mapigano makali baina ya vikosi vya Marekani na vya wanamgambo wa kitalibani.Miongoni mwa visa vyengine,msafara wa mazishi ulishambuliwa kwa mabomu.Kisa hiki yadhihirika, ni sababu iliompeleka muandishi huyo wa kijerumani kwenda huko kutafuta ukweli.

Madai ya watekanyara bado hayajulikani.Kwa muujibu wa serikali ya mkoa,yamkinika wataliban au wahalifu wamehusika .Kwa muujibu wa kituo cha kwanza cha TV cha Ujerumani ARD kivyoarifu yamkini wakereketwa wa mbabe wa vita na waziri mkuu wa zamani Hekmatyar wamehusika.

Hekmatyar,muislamu mwenye itikadi kali ana mafungamano na Al kaida.Kuna ni moja