1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUNICH: Mkutano wa CSU kuchagua mrithi wa Stoiber

29 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLj

Wahafidhina katika jimbo la Bavaria,kusini mwa Ujerumani hii leo wanamchagua mrithi wa Edmund Stoiber aliekuwa mwenyekiti wa chama cha Christian Social Union-CSU.Stoiber pia anamaliza awamu ya miaka 14 kama waziri mkuu wa jimbo la Bavaria baada ya kushinikizwa na wanachama wenzake kwa miezi kadhaa.

Günther Beckstein ambae hivi sasa ni Waziri wa Ndani wa Bavaria anamrithi Stoiber kama waziri mkuu wa jimbo hilo.