1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaka mmoja tangu kutokea vita vikali kati ya Hezbollah na Israel

12 Julai 2007

Mamia ya walebanon waliuwawa kwenye mashambulio ya angani yaliyofanywa na Israel kwa kisingizio cha kuwalenga Hezbollah.Majumba mengi yaliharibiwa.

https://p.dw.com/p/CB2t
Mabomu ya Israel yakivurumishwa dhidi ya makazi ya walebanon
Mabomu ya Israel yakivurumishwa dhidi ya makazi ya walebanonPicha: AP

Lebanon leo hii inaadhimisha mwaka mmoja tangu kutokea mapigano makali baina ya Hezbollah na Israel mapigano ambayo yalisababisha uharibifu mkubwa nchini Lebanon.

Waziri mkuu Fuad Siniora amewataka walebanon kuondoa tafauti zao za kisiasa na kuunga mkono wanajeshi ambao wamekuwa katikati ya mapambano na wapiganaji wenye siasa kali wa kisunni kaskazini mwa nchi hiyo kwa zaidi ya siku 50 sasa.

Kumekuweko na mivutano ya kisiasa nchini Lebanon kati ya serikali ya Siniora na kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Syria.

Duru zilizokaribu na Hezbollah zinaarifu kila eneo lililoathiriwa na mashambulio ya Israel litaandaa sherehe zake ndogo kuadhimisha siku hii ili kuepuka mkusanyiko mkubwa wa watu kutokana na sababu za kiusalama.