1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa Ivory Coast

5 Desemba 2010

Nchi moja, Marais wawili ndivyo hali ilivyo nchini Ivory Coast. Wagombea wote wawili wa urais waapishwa, huku hali ya wasiwasi ikongezeka.

https://p.dw.com/p/QQ43
Rais Laurent Gbagbo, aliapishwa jana.Picha: AP

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki amewasili nchini Ivory Coast kujaribu kuleta upatanishi katika mzozo wa uchaguzi ambao ulitarajiwa kumaliza mzozo uliodumu nchini humo kwa muongo mmoja, lakini badala yake umeufanya mzozo huo kuwa mgumu zaidi. Hii ni baada  ya  wagombea urais  wote  kuapishwa. Rais  wa   sasa  Laurent  Gbagbo  aliapishwa, licha ya tume ya uchaguzi kumtangaza Alassane Ouattara kama mshindi.   Hata  hivyo baada  ya  muda  wa  saa  kadha, Ouattara  ambaye ni mgombea wa upinzani naye  pia  alidai  kuwa  rais. Marekani, Umoja  wa  Ulaya  na  Umoja  wa Mataifa  kwa  pamoja   zimesema  kuwa  mshindi wa uchaguzi  wa  Jumapili iliyopita ni  Ouattara. Ouattara alitangazwa  mshindi na tume ya uchaguzi lakini   hatua  hiyo  ilibatilishwa  na  baraza  la  katiba   la  nchi  hiyo, taasisi ambayo  inaongozwa  na  mshirika  wa  rais  Gbagbo.  Uchaguzi  huo ulikuwa  na  lengo  la   kupoza  majeraha  ya  vita  vya  wenyewe  kwa wenyewe  vya  mwaka  2002, lakini  badala  yake  unatishia  kuanzisha  upya hali  ya  wasi  wasi