1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Naibu waziri wa nje wa Marekani ziarani nchini Somalia

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBP

BAIDOA:


Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani,anaeshughulikia masuala ya Afrika,JENDAYI FRAZER amekwenda Somalia kwa mazungumzo pamoja na viongozi wa seerikali ya mpito.Lengo ni kuhimiza juhudi za kuweka chini silaha kuweza kuitishwa mazungumzo ya suluhu.Mara baada ya kuwasili bibi JENDAYI FRAZER amekutana na rais ABDULLAHI YUSUF,waziri mkuu Ali Mohammed GEDI na wakuu wa bunge la Somalia.Mwanadiplomasia huyo ni afisa wa kwanza wa ngazi ya juu wa Marekani kuitembelea Somalia tangu mwaka 1994.Ziara yake imesadifu siku sita baada ya kutiwa njiani makubaliano tete ya kuweka chini silaha baada ya mapigano makali yaliyoutikisa mji mkuu Mogadischu.Mkutano wa suluhu ya taifa umepangwa kuitishwa April 16 ijayo.