1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Mataifa ya maziwa makuu yakutana kutia saini makubaliano kuhusu maendeleo.

14 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjc

Marais 11 wa mataifa ya Afrika wamealikwa katika mji mkuu wa Kenya nairobi leo kwa ajili ya mkutano wa kimataifa wenye lengo la kuimarisha juhudi za kuimarisha eneo tete la maziwa makuu barani humo.Mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu eneo la maziwa makuu, ambao umefunguliwa siku ya Jumatatu ukihudhuriwa na mawaziri wa bara hilo, utamalizika kwa mkutano huo katika makao makuu ya umoja wa mataifa.Mawaziri hao wanakamilisha muswada wa azimio litakalowasilishwa katika mkutano wa marais hao, ambapo wanachama wa kundi la mataifa ya maziwa makuu wanatarajiwa kutia saini mkataba unaohimiza amani katika eneo hilo pamoja na maendeleo.Mkataba huo pia utajumuisha kuundwa kwa mfuko maalum wa ujenzi mpya na maendeleo , utakaoungwa mkono na mataifa wanachama Angola, Burundi, jamhuri ya Afrika ya kati, jamhuri ya Kongo, jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, Kenya, Rwanda, Sudan, Tanzania, Uganda na zambia.