1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Mkutano wa maziwa makuu wafunguliwa

14 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjQ

Licha ya mafanikio ya kidemokrasia ya hivi karibuni katika nchi za Maziwa Makuu barani Afrika mengi bado yanahitajika kufanywa kulinda usalama na maendeleo katika mojawapo ya maeneo yenye umwagaji mkubwa wa damu duniani.

Eneo hilo la kimaskini ambalo miongoni mwa nchi inazozijumuisha ni pamoja na Uganda,Rwanda,Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo limekuwa kwenye matatizo ya umwagaji damu tokea mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 ambayo nayo yamechochea vita kadhaa na vile vya kujibu mapigo.

Marais sita wa Afrika wako nchini Kenya kwa mazungumzo hayo juu ya usalama,utawala bora na maendeleo ya kiuchumi wamepongeza chaguzi za kihistoria katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na utulivu nchini Burundi kufuatia kipindi cha vita.

Rais Jakaya Kikwete aliufunguwa mkutano huo akiwa na matumaini makubwa.Marais wengine waliohudhuria mkutano huo ni wenyeji Kenya, Uganda, Burundi,Congo,Zambia na waziri mkuu wa Rwanda.