1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Jamaa wa washukiwa wa ugaidi wazuiliwa kuandamana

19 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOc

Polisi nchini Kenya waliwazuia jamaa wa raia 18 wa Kenya wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya ugaidi kuandamana ili waachiwe kutoka Ethiopia wanakoshukiwa kuzuiliwa.Wanaharakati na jamaa hao walipanga kuandamana hapo jana hadi majengo ya bunge na ubalozi wa Ethiopia ili kuwasilisha maombi rasmi ya kudai kuachiwa kwa raia 18 wa Kenya.Hatua hiyo inatokea baada ya takriban waislamu alfu 3 kuandamana Ijumaa iliyopita ili kupinga hatua ya serikali ya kuwapeleka washukiwa wa ugaidi katika mataifa mengine ili kuchunguzwa.

Hata hivyo polisi waliowasiliana na jamaa hao kwa barua waliwaruhusu kufanya mkutano katika eneo la Freedom Corner mjini Nairobi.Eneo hilo lilitumika kwenye kampeni za kudai kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa katika miaka ya tisini.Maafisa wa serikali wa Ethiopia walikataa kusema chochote kuhusiana na tukio hilo.Kulingana na mwenyekiti wa Kundi la kutetea haki za waislamu Muslim Human Rights Forum Bwana Abdullahi Yusuf kundi hilo linapanga kufanya maandamano mengine wiki hii.