1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAJAF: Maelfu waandamana nchini Irak kupinga uvamizi wa Marekani

9 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCB3

Maelfu ya watu wameshiriki katika maandamano makubwa kupinga uvamizi wa Marekani katika mji mtakatifu wa Najaf ulio kusini mwa Irak.

Waandamanaji hao kwa sauti za juu waliimba miito ya kulaani kuwepo wanajeshi wa Marekani nchini Irak baadhi ya waandamanaji hao walichoma bendera za Marekani.

Kiongozi mbishi wa madhehebu ya Shia Moqtada al Sadr aliwataka wafuasi wake kufanya maandamano kuadhimisha miaka minne tangu kuangushwa utawala wa Saddam Hussein na tangu Irak kuingia mikononi mwa wanajeshi wa Marekani.

Amri ya saa 24 imetolewa ambako magari hayaruhusiwi kutembea katika mji wa Baghdad, amri hiyo imetolewa ili kudhibiti mashambulio katika siku hii ya maadhimisho.