1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Baraza la Umoja wa Mataifa laongeza muda wa majeshi yake nchini Ivory Coast.

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbn

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kuongeza muda kufikia tarehe thelathini mwezi Juni kwa vikosi vyake na pia vya Ufaransa vinavyolinda amani nchini Ivory Coast.

Wanajeshi zaidi ya elfu nane wa Umoja wa Mataifa na wengine elfu nne wa Ufaransa wamekuwa nchini humo tangu mwezi Novemba mwaka uliopita kuhakikisha kutekelezwa mwafaka wa amani kati ya majeshi ya serikali ya Rais Laurent Gbagbo na vikosi vya waasi.

Baraza hilo limewataka wanajeshi hao kusaidia kuyavunja makundi ya waasi na pia kusaidia katika maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanywa tarehe thelathini na moja mwezi Oktoba mwaka huu.