1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Baraza la usalama laidhinisha azimio kuunda mahakama.

31 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwO

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeidhinisha azimio litakalounda mahakama ya kimataifa itakayowahukumu watuhumiwa wa mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri.

Waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora amelitaka baraza hilo mapema mwezi huu kuunda mahakama hiyo.

Azimio hilo linatoa kwa bunge la Lebanon nafasi ya mwisho ya kuendesha kesi hiyo.

Iwapo haitachukua hatua hadi ifikapo Juni 10 , makubaliano ya umoja wa mataifa na Lebanon yanaweza kuunda mahakama hiyo nje ya Lebanon chini ya mwendesha mashtaka wa kimataifa na majaji.