1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Hatua zichukuliwe haraka kuzuia muongezeko wa joto duniani

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVU

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa,kuchukuwa hatua za haraka kupambana na tatizo la muongezeko wa joto la ardhi.Ban ametamka hayo baada ya jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa kutoa ripoti inayotisha kuwa mabadiliko ya hali ya hewa duniani,yamesababishwa na binadamu.Wanasayansi hao vile vile wamesema,hali hiyo inazidi kuwa mbaya kwa sababu ya matumizi ya fueli ya visukuku.Serikali za Marekani na Australia,ambazo hazikutia saini Mkataba wa Kyoto unaotoa wito wa kupunguza uchafuzi wa mazingira,hazikuitia sana maanani ripoti ya Umoja wa Mataifa.Waziri wa nishati wa Marekani,Sam Bodman amedai kuwa Marekani inayotoa robo ya gesi ya kaboni dayoksaidi duniani,ni mchangiaji mdogo wa madhara yaliotokea.Wakati huo huo waziri wa mazingira wa Australia,Malcolm Turnbull amesema,nchi yake itatia saini Mkataba wa Kyoto unaoweka viwango vya gesi inayochafua mazingira,ikiwa masharti hayo yanaweza kutekelezwa kiuchumi.Kundi linalogombea kuhifadhi mazingira - “Marafiki wa Dunia“ - limetoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuamrisha kupunguza kwa asilimia 30,gesi inayochafua mazingira.