1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Umoja wa Mataifa wafadhaishwa na mzozo wa Somalia.

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea kufadhaishwa na mzozo unaoendelea nchini Somalia.

Balozi wa Russia wa Umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin, amewaambia waandishi wa habari baada ya mkutano wa faragha kwamba nchi wanachama wa baraza hilo zinaunga mkono kupelekwa haraka iwezekanavyo wanajeshi wa Umoja wa Afrika wa kulinda amani nchini Somalia.

Baraza hilo pia limeunga mkono mpango wa Umoja wa Mataifa wa kupeleka kundi la wataalamu kutathmini misaada ya kibinadamu inayohitajika nchini humo.

Mjumbe wa Marekani, Jackie Sanders, alisema alilipatia baraza hilo taarifa kuhusu shambulio lililofanywa siku ya Jumatatu nchini Somalia likiwalenga wafuasi wa kundi la al Qaeda.

Bi Jackie Sanders alisema hatua hiyo ya Marekani haikukabiliwa na upinzani wowote kwenye mkutano huo.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametahadharisha huenda hatua hiyo ya Marekani ikazidisha ghasia.