1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Venezuela inakataa kugombea kiti katika baraza la usalama

18 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1f

Venezuela inakataa kuwachilia kugombea kiti cha Latin Amerika katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Baada ya siku mbili na raundi 22 za upigaji kura, Venezuela haijashinda raundi hata moja dhidi ya Guatemala.

Lakini Guatamela imeshindwa kupata thuluthi mbili ya kura inazotakikana kushinda.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa litapumzika kupiga kura leo na kuanza kupiga kura tena hapo kesho.