1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Jenerali wa Rwanda atuhumiwa kutumia vibaya mamlaka

23 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWp


Umoja wa Mataifa umesema Jenerali wa Rwanda aliechaguliwa kuongoza jeshi la kulinda amani katika jimbo la Darfur amelaumiwa kwa kutumia mamlaka yake vibaya kuhusiana na wafungwa wakati ambapo mauaji halaiki yalitendeka nchini Rwanda.

Jenerali huyo Karenzi Karake aliteuliwa hivi karibuni kuwa naibu mkuu wa jeshi la pamoja baina ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika linalokusudiwa kupelekwa Darfur magharibi mwa Sudan ili kukomesha mauaji.

Sasa madai yameibuka kwamba afisa huyo wa kabila la kitusi alitumia vibaya mamlaka yake dhidi ya wahutu waliokuwa mahabusu.

Watu laki nane waliangamia katika mauaji halaiki nchini Rwanda mnamo mwaka 1994.