1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEY YORK: Ban Ki Moon kulipa uzito ongezeko la joto duniani

2 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNF

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha hatari kubwa kwa ulimwengu kama vita.

Akiwahutubia wanafunzi katika baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Ban Ki Moon ameitolea mwito Marekani iongoze juhudi za kukabiliana na ongezeko la joto duniani.

Kiongozi huyo amesema ipo haja ya kuunda mkakati madhubuti wa kukabiliana na maswala ya kimazingira.

Mwezi uliopita jopo la wanasayansi wa mazingira liliwasilisha ripoti iliyooonya juu ya ukame, kuongezeka kwa kima cha maji baharini na joto kali. Ripoti hiyo pia ilimlaumu binadamu kwa kusababisha ongezeko la joto duniani.