1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Oparesheni: Jeshi la Marekani lawaua Wanamgambo 8

Eric Kalume Ponda22 Desemba 2008

Nchini Afghanistan oparesheni ya pamoja ya jeshi la Marekani na Afghabnistan katika eneo la mpakani mwa nchi hiyo na Pakistan, limewauawa wapiganaji 8 wanaoaminika kuwa wafuasi wa makundi ya Kitaliban na Al-Qaeda.

https://p.dw.com/p/GLWK
Wanajeshi wa Marekani wanaoendesha oparesheni nchini Afghanistan.Picha: AP


Shambulizi hilo la makombora mawili kutoka kwa vikosi vya jeshi la Marekani, lilishambulia eneo linaloaminika kuwa ngome ya makundi ya wapiganaji katika eneo la Kazkasini magharibi mwa Pakistan linalopakana na Afghnaistan.Hata hivyo shambulizi hilo huenda limechochea zaidi kuzorota kwa uhusiana baina ya Pakistan na Marekani


Makombora hayo mawili yalishambulia vijiji viwili vya Karikot na Shin Warsak katika eneo linalokumba na ghasia la Waziristan Kusini,katika juhudi za hivi punde kabisa za vikosi vya Marekani dhidi ya makundi ya kigaidi eneo hilo.


Maafisa wa jeshi la Marekani walisema kuwa magari mawili makundi hayo ya kigaidi yalikuwa na silaha kali yaliharibiwa kabisa wakati wa shambulizi hilo. Hata hivyo haikubainika mara moja iwapo mafisa wa ngazi za juu wa makundi ya kigaidi ya AlQaeda au Taliban waliuawa kwenye mashambulizi hayo mawili yaliyotekelezwa kwa pamoja.


Shambulizi hilo limetokea huku Marekani ikijiandaa kupeleka wanajeshi zaidi kukabiliana na makundi hayo ya kigaidi hapo mwakani. Msemaji wa jeshi la Marekani nchini Afghanistana Jerry O´Hara, alisema kuwa makundi ya kigaidi ambayo yameimarisha harakati zao katika siku za hivi majuzi zinatishia usalama kote ulimwenguni.



Oparesheni hiyo imetekelezwa licha ya onyo kali kutoka kwa makundi ya wapiganaji wa Kitaliban nchini Pakistan kwamba shambulizi lolote dhidi yao litajibiwa vikali kutoka upande wa Pakistan. Hii ni kufuatia shambulizi la mwezi uliopita lililotekelezwa na Jeshi la Marekani ambalo lilisababisha kuuawa kwa kiongozi mmoja wa kundi la Al-Qaeda Rashid Rauf anayeaminika alipanga shambulizi dhidi ya ndege moja ya shirika la Trans Atlantic mwaka wa 2006.


Jumla ya wapiganaji 20 wameuawa tangu mwezi uliopita kufuatia oparesheni kali ya jeshi la Marekani katika eneo hilo.


Hata hivyo serikali ya Pakistan imeshutmu vikali oparesheni hiyo katika ardhi yake bila ya kuhusishwa. Waziri mkuu wa nchi hiyo Ahmed Schah Ahmed amesema kuwa opareshi hiyo inamadhara makubwa kwa raia wa taifa hilo wasio na hatia.


Serikali ya Pakistan imekuwa ikishinikizwa na jamii ya kimataifa kukabiliana na makundi ya kigaidi yenye makao yao nchini humo, hali iliyopelekea wa rais wa Asif Al Zadari kutoa hakikisho kwamba serikali yake imejitolea kuangamiza kabisa makundi ya kigaidi nchini humo.


Rais Al Zardari alitoa hakikisho hilo kufuatia sham bulizi la kigaidi lililotekelezwa dhidi ya vituo vitano vilivyoshambuliwa mwezi uliopita nchini India


Marekani imeimarisha oparesheni zake za kijeshi nchini Pakistan ambako kiongozi wa kundi la kigaidi la AlQaeda Osama Bin Laden yaaminika amejificha. Hata hivyo makamu wa rais wa Marekani Dick Cheney alisema mwishoni mwa wiki, kuwa hana uhakika iwapo Osama Bin Laden anayeshtumiwa kwa shambulizi la Septemba 11 2001 nchini Marekani yungali hai.