1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Oxfam: Matajiri wachache wanachafua mazingira

Sudi Mnette
21 Septemba 2020

Ripoti mpya ya Shirika la Hisani la Oxfam inasema asilimia moja ya matajiri inahusika na uchafuzi wa mazingira mara mbili ya kile kiwango kinachozalishwa na nusu idadi ya idadi jumla ya watu masikini duniani.

https://p.dw.com/p/3ilYl
Hunger im Sahel Bildergalerie Tschad
Picha: Andy Hall/Oxfam

Ripoti hiyo inatolewa kabla ya Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa. Shirika hilo limetoa wito wa kuweka vizuizi vya kudhibiti uzalishaji wa kaboni miongoni mwa matajiri, uwekezaji zaidi katika miundombinu ya umma na uchumi uundwe kwa namna bora ya kuzingatia mabadiliko ya taiubia nchi.

Ripoti hiyo ilijikita katika data zilitzokusanywa kati ya 1990 na 2015, kipindi ambacho uchafuzi wa mazingira uliongezeka maradufu duniani kote. Ripoti imebaini asilimia 10 ya watu matajiri zaidi ikiwa sawa na watu 630 wanahusika moja kwa moja na uchafuzi wa zaidi ya nusu (52%) ya utoaji wa hewa ya kaboni katika kipindi hicho. Asimia nyingine moja ya watu matajiri ikiwa sawa na watu 63 wanahusika kwa asilimia 15 ya uchafunzi wa mazingira.

Kiwango cha joto bado kipo juu duniani

Blick vom Fernsehturm Colonius in Köln
Moja ya kiwanda mjini Cologne UjerumaniPicha: Christoph Hardt/Geisler-Fotopress/dpa/picture alliance

Pamoja na kupungua kwa kasi gesi ya kaboni kulikotokana na janga la virusi vya corna, lakini bado ulimwengu umesalia katika kiwango kilekile cha ongezeko la joto katika karne hii.

Mtaalamu wa masuala ya usawa wa kijamii wa Oxfam kwa Ujerumani Ellen Ehmke amesema matokeo mabaya la janga la mabadiliko ya tabia nchi tayari limeanza kushuhudiwa katika maeneo tofauti ya ulimwengu. Anasema idadi kubwa ya watu masikini wanatabika kutokana na furaha ya matajiri wachache. Kwa kuzingatia hapa Ujerumani kwa mfano utafiti huo unaonesha asilimia 10 ya matajiri ambao sawa na watu milioni 8.3 wanahusika na uchafuzi wa asilimia 26 ya gesi ya kaboni, katika kipindi hicho ambacho utafiti huo wa Oxfam ulifanyika.

Soma zaidi: Ripoti ya Oxfam: Wanawake hufanya kazi bure wakati mabilionea wakiongeza utajiri

Nusu ya idadi ya watu masikini nchini humu, ambao inafanya mara tano ya matajiri, ikiwa sawa na watu milioni 41.5 wanachangia uchafuzi mdogo sana wa kuzidi kidogo asilimia 29. Msongamano wa magari, usafiri wa angani moja kati ya mambo muhimu yanayochangia mabadiliko ya tabia nchi. Kwa namna ya kipekee shirika la Oxfam limekosoa matumizi ya magari makubwa ya familia, kwa kusema yameongoza kwa kushika nafasi ya pili kwa uchafuzi wa mazingira kati ya 2010 na 2018.

Vyanzo AFP/DPA