1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Chirac asisitiza umuhimu wa kuzuia muongezeko wa joto duniani

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVS
Waziri Mkuu wa Israel, Ehud Olmert
Waziri Mkuu wa Israel, Ehud OlmertPicha: AP
Rais Jacques Chirac wa Ufaransa ametoa wito wa kuunda Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa.Alitamka hayo mjini Paris wakati wa kufunga mkutano uliotoa ripoti inayotia hofu kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani.Chirac amesema,kuna haja ya kuwa na shirika maalum litakalorithi “Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa“ kupambana na tatizo la muongezeko wa joto la ardhi pamoja na uharibifu mwingine wa sayari yetu.