1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Waziri mkuu wa zamani afikishwa mahakamani

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBei

Waziri mkuu wa zamani nchini Ufaransa Dominique de Villepin anaganyiwa uchunguzi kwa madai ya kuhusika na njama ya kumuharibia jina Rais Nikolas Sarkozy iliyolenga kutia dosari uwezo wake kushinda urais.Bwana Villepin alifika kwenye afisi za majaji Jean-Marie d’Huy na Henri Pons hii leo ili kujibu maswali lakini kuondoka baada y akuarifiwa kuwa anafanyiwa uchunguzi.Hatua itakayofuatia ni kujibu mashtaka.

Bwana de Villepin amesema hakuna hata wakati mmoja aloshiriki katika njama ya kisiasa

Bwana Villepin alisema atashirikiana na mahakama ila hakuhusika na kashfa ambayo jina la Rais Sarkozy liliorodheshwa kwenye akaunti bandia za benki kwenye benki moja nchini Luxembourg.Kiongozi huyo wa zamani aliitwa tena mahakamaji baada ya ushahidi mpya kutolewa na afisa wa zamani wa ujasusi Phillipe Rondot.