1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Kenya watawanya maandaano ya wafuasi wa rais Kibaki

22 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cvwh

NAIROBI:

Polisi ya Kenya imetumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa rais Mwai Kibaki waliokuwa wanaandamana mjini Nairobi kuunga mkono kuchaguliwa tena kwa Bw Kibaki.

Polisi imewafukuzana na waandamanaji katika barabara kadhaa pamoja na maduka mjini humo.Waandamanaji walikuwa wakipiga makelele wakisema kuwa KIbaki endelea mbele.

Polisi imepiga marufu mikutano na maandamano yote nchini humo tangu uchaguzi wa mwezi jana.maandamano karibu ya mwanzo ilikuwa inafanywa na upande wa upinzani. Polisi imewarushia gesi ya kutoa machozi watu wapatao 100 walipokuwa wakitembea katika barabara za mjini Nairobi.

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa.Koffi Annan pamoja na rais Yoweri Museveni wametarajiwa kufika nairobi leo kujaribu kupatanisha pande husika katika mgogoro ulioanza Desemba 27 wakati upinzani ulidai kuwa kulifanyika mizengwe.