1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRAGUE:Bush amnyooshea mkono wa ushirikiano Putin

5 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuY

Rais George Bush wa Marekani ameialika Urusi katika mpango wake wa kuweka makombora ya kujihami Ulaya ya Mashariki.

Akizungumza mjini Prague baada ya kukutana na viongozi wa Jamhuri ya Czech, alielezea kushangazwa kwake na Urusi kutoshiriki katika mpango huo.

Urusi inaupinga mpango huo, ambapo Marekani imepanga kuweka makombora hayo katika nchi za Poland na Czech, ikionya kuwa nayo itaelekeza makombora yake ulaya.

Aidha Rais Bush alisema nchi hiyo haina uadui na Urusi.

Rais Bush na Rais Vladmir Putin wanatarajiwa kuwa na mazungumzo ya faragha pembezoni mwa mkutano wa wakuu wa nchi za G8 unaoanza kesho huko Hailegendamm Ujerumani.