1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG:Rais wa Korea Kusini awasili Korea Kaskazini kwa mazungumzo

2 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKo

Marais Roh Moo-Hyun wa Korea Kusini na Kim Jong-Il wa Korea Kaskazini wameanza mkutano wao wa ujirani mwema mjini Pyongyang.

Huo ni mkutano wa pili kihistoria kwa wakuu wa nchi hizo mbili toka mwaka 2000.

Mapema wakati akiwasili Korea Kaskazini Rais huyo wa Korea Kusini alivuka mpaka wa nchi hizo mbili kwa mguu ikiwa ni ishara ya maridhiano kati ya nchi hizo mbili hasimu, ambapo alipokewa na mwenyeji wake.

Mkutano huo wa wakuu hao unaongeza hatua katika mazungumzo ya pande sita juu ya Korea Kaskazini kufunga vinu vyake vya nuklia.

Wawakilishi katika mazungumzo hayo hapo siku ya jumapili walifikia makubaliano ya awali juu ya awamu ya pili ya mpango wa nchi hiyo kuacha utengezeji wa silaha za nuklia.