1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa kike wa kwanza ameapishwa Argentina

11 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZyV

Cristina Fernandez de Kirchner ameapishwa kama rais wa kike wa kwanza nchini Argentina.Kirchner alie na umri wa miaka 54 aliapishwa mbele ya mabaraza mawili ya Bunge.Katika uchaguzi uliofanywa mwezi wa Oktoba,Kirchner alishinda asilimia 45 ya kura zilizopigwa.

Cristina Fernadez de Kirchner anachukua nafasi ya mume wake,Nestor Kirchner anaeondoka madarakani baada ya kumaliza muhula mmoja wa miaka minne kama rais.