Rais Medvedev ataka usalama uimarishwe Urusi
25 Januari 2011Matangazo
Kiasi ya watu 35 waliuawa na wengine 150 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.Kwa mujibu wa msemaji wa uwanja wa ndege wa Domodyedova,mlipuko huo ulitokea kwenye ukumbi wanakowasili maelfu ya abiria wa kimataifa.Muda mfupi baada ya mkasa huo,rais wa Urusi Dmitry Medvedev alimuru usalama uimarishwe katika vituo vyote vya usafiri nchini humo na akaahidi kuwa wahalifu waliohusika watakamatwa. Hata hivyo,mpaka sasa hakuna kundi lolote lilokiri kuhusika na shambulio hilo ijapokuwa mji mkuu wa Urusi wa Moscow umekuwa kwa miaka mingi, shabaha ya wapiganaji wa kiislamu wanaotokea eneo la milima ya Kaskazini.
Mwandishi:Thelma Mwadzaya
Mpitiaji:Hamidou Oummilkheir