1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais mpya wa EU apongezwa

Aboubakary Jumaa Liongo20 Novemba 2009

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamejipongeza baada ya kumteua Waziri Mkuu wa Ubelgiji Herman Van Rompuy kuwa rais wa kwanza wa Jumuiya hiyo.

https://p.dw.com/p/Kbxa
Rais mpya wa Umoja wa Ulaya Herman Van RompuyPicha: AP

Katika majadiliano hayo ya faragha ambayo yalidumu kwa siku nzima viongozi hao wa ngazi za juu pia walimteua Kamishna wa Umoja huo Baronnes Cathy Ashton kuwa mwakilishi mkuu wa sera za kigeni.

Punde baada ya saa tatu usiku hapo jana Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya aliye pia Waziri mkuu wa Sweden Fredrik Reinfeldt alimtangaza rasmi rais mteule wa Jumuiya hiyo Waziri Mkuu wa Ubelgiji Herman van Rompuy pamoja na mwakilishi mkuu wa sera za kigeni  Baronnes Cathy Ashton wa Uingereza aliyekuwa Kamishna wa masuala ya biashara.m,wenyekiti wa Umoja wa Ulaya Fredrik Reinfeldt alifurahishwa na uteuzi huo.

´´Tulichokuwa tukikitafuta ni watu watakaoweza kuendeleza sera zetu ili tuweze kuungana kwa lengo la kuwa sauti ,sura na wawakilishi wa bara la Ulaya kote ulimwenguni.Jee tumelitimiza hilo?ndio nadhani tumelitimiza.´´   

Uteuzi huo una maana kuwa washindi katika Baraza la Umoja wa Ulaya ni wale waliokuwa wakiunga mkono uteuzi wa mtendaji badala ya kiongozi atakayekuwa ana tajika sana.Van Rompuy alilitimiza hilo na kauli alizotoa baada ya kuteuliwa ziliashiria hilo.

´´Mtazamo wangu ni kuwa mtazamo wa Baraza haujalishi chochote.Haijalishi ninachokifikiria mimi.Wajibu wangu ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na uwiano´´. 

Bibi Ashton aliweka rekodi mpya tena kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo ya ngazi za juu ijapokuwa hana uzoefu katika masuala ya sera za kigeni.Baronnes Ashton alizipinga viklai dhana hizo

´´Naamini kwamba uzoefu wangu utabainika waziwazi.Jee mimi ni kama tai?La hasha?Jee natakla kuonekana kuwa nataka kuzungumza kila wakati?La hasha.Ni bora kupitisha maamuzi  baada ya kuutathmini utendaji wangu na naamini mtafurahi na mtajivunia.´´

Kiongozi wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso aliyekuwako wakati wa shughuli hiyo alisema kuwa lile suala la kuwa na kiongozi atakeliwakilisha bara la Ulaya sasa limepata suluhu.Itakumbukwa kuwa Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Marekani Henry Kissinger alilizusha suali hilo wakati alipokuwa uongozini.Raisi mteule wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy kwa upande wake alisema kuwa anasubiri kwa hamu kuipokea simu ya kwanza kuhusu masuala ya Jumuiya hiyo.

Kwa upande wao huo viongozi wa bara la Ulaya wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu uteuzi huo mpya.Kwa mujibu wa kiongozi wa chama cha mazingira katika Bunge la Umoja wa Ulaya Daniel  Cohn-Bendit uteuzi huo umezidi kuzimaliza nguvu taasisi za Umoja huo.Hata hivyo Marekani imeupongeza uteuzi huo.Rais Barack Obama amesema kuwa uteuzi huo utalifanya bara la Ulaya kuwa mshirika thabiti zaidi.

Ujerumani kwa upande wake nayo imeipongeza hatua hiyo.Hata hivyo mitazamo tofauti bado itaendelea kuwepo hata baada ya uteuzi huu.Hii ni kwasababu Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya bado anaendelea na majukumu yake,Bunge la Umoja wa Ulaya nalo pia litaendelea na majukumu yake vilevile mfumo wa Mwenyekiti wa zamu bado pia nao utaendelea.

Mwandishi:Thelma Mwadzaya/ZPR/C Hasselbach

Mhariri:Abdul-Rahman