1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Pervez Musharraf kuapishwa leo kuwa rais wa kiraia

29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUPL

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan ataapishwa leo kuwa rais wa kiraia.

Rais Musharraf ataapishwa siku moja baada ya kujiuzulu wadhifa wake kama kamanda mkuu wa jeshi la Pakistan katika makao makuu ya jeshi mjini Rawalpindi, hivyo kumaliza miaka minane ya utawala wa kijeshi nchini humo.

Rais Musharraf amekabidhi madaraka ya jeshi kwa jenerali Ashfaq Kiyani.

Rais George W Bush wa Marekani ameisifu hatua ya rais Musharraf kujiuzulu wadhifa wake jeshini lakini akarudia miito ya jumuiya ya kimataifa inayomtaka aondoe utawala wa hali ya hatari nchini Pakistan kabla uchaguzi kufanyika hapo tarehe 8 mwezi Januari mwakani.

Aidha rais Bush amesema hiyo ndiyo njia pekee kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa uhuru na haki.