1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani Wulff atoa ujumbe wa Krisimasi

Mtullya Abdu24 Desemba 2011

Rais wa Ujerumani Christian Wulff ametoa mwito wa kuwapo jamii ya uwazi nchini Ujerumani. Amesema, nchini Ujerumani hakuna nafasi ya chuki dhidi ya wageni, matumizi ya nguvu na siasa za mrengo mkali.

https://p.dw.com/p/13Yjb
(ACHTUNG - SPERRFRIST: Die Bilder sind freigegeben für Online-Verwendung ab 24.12.2011, 0:01 Uhr.) Bundespräsident Christian Wulff steht am Mittwoch (21.12.2011) in Berlin bei der Aufzeichnung der Weihnachtsansprache des Bundespräsidenten vor einem Christbaum. Foto: Bundespresseamt/Jesco Denzel +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais wa Ujerumani Christian WulffPicha: picture-alliance/dpa

Rais Wulff ameyasema hayo kuhusiana na mfululizo wa mauaji yaliyofanywa na kundi la mafashisti mamboleo katika jimbo la Thuringia, mashariki mwa Ujerumani.
Rais wa Ujerumani amesema, matukio hayo yaliyokuwa na hulka za uhalifu wa kibaguzi yaliwashtua watu wote.
Katika ujumbe wake Rais Wulff pia amewataka watu wawe macho na tayari kutetea demokrasia, maisha na uhuru wa wananchi wote wa Ujerumani.
Rais wa Ujerumani pia alizungumzia juu ya mgogoro wa madeni barani Ulaya na amewataka watu wawe na moyo.
Amesema, ana uhakika kwamba itawezekana kupatikana njia ya kuufumbua. Pia amehakikisha kwamba Ujerumani itaendelea kuwa na msimamo wa mshikamano barani Ulaya.