1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Maduro aafiki kufunguliwa tena kwa ofisi ya haki ya UN

24 Aprili 2024

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametangaza kuwa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu itaanza tena kufanya kazi nchini humo.

https://p.dw.com/p/4f75P
Venezuela-Caracas | Rais Nicolas Maduro
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro Picha: Zurimar Campos/AFP

Ofisi hiyo ilifungiwa na wafanyakazi wake kuamriwa kuondoka mnamo mwezi Februari mwaka huu.

Maduro aliitoa kauli hiyo akiwa pamoja na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, Karim Khan ambaye alikuwa ziarani katika mji mkuu wa Venezuela, Caracas.

Soma pia: Upinzani Venezuela wamsajili mgombea wa uchaguzi wa rais      

Mabadiliko hayo ya msimamo yanajiri huku Maduro akikabiliwa na mzozo wa ndani na nje ya nchi kuhusu rekodi ya serikali yake ya mrengo wa kushoto katika masuala ya haki za binaadamu, pamoja na kuukandamiza upinzani wakati akitazamiwa kuwania muhula wa tatu madarakani.