1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Yemen yutayari kujiuzulu kwa masharti

25 Aprili 2011

Kwa mujibu wa habari rasmi, Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh anaetawala tangu miaka 32 iliyopita yupo tayari kujiuzulu baada ya serikali yake kukubali pendekezo lililotolewa na Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba GCC.

https://p.dw.com/p/RK40
Yemeni President Ali Abdullah Saleh speaks to a meeting of security commanders in the capital Sana', Yemen, 24 January 2009. President Saleh said Yemen would receive 94 inmates who are to be released from the military prison at the U.S. military base in Guantanamo within two to three months, addingthat his country had rejected a US proposal to send the Yemeni detainees from Guantanamo to Saudi Arabia to be rehabilitated. EPA/YAHYA ARHAB +++(c) dpa - Report+++
Rais wa Yemen, Ali Abdullah SalehPicha: picture-alliance/ dpa

Kimsingi, pendekezo hilo la GCC limekubaliwa pia na vuguvugu la upinzani, lakini hiyo jana maandamano yalifanywa upya katika mji mkuu, Sanaa. Mapambano ya umwagaji damu kati ya Rais wa Yemen, Ali Abdullah Saleh, na vuguvugu la upinzani linaendelea kwa takriban miezi miwili nchini humo, lakini kuna uwezekano wa mapigano hayo kumalizika. Kwani kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, Rais Saleh, kimsingi, amekubali pendekezo lililotolewa na nchi za Ghuba. Naibu waziri wa habari, Abdu al Janadi, alipozungumza na Al Jazeera, alieleza hivi:

"Rais na chama tawala wanaunga mkono vifungu vyote vya pendekezo hilo. Na hilo litatekelezwa kuambatana na katiba ya Yemen."

Kipengele muhimu katika pendekezo hilo ni kuwa Rais Saleh na wafanya kazi wa zamani na wa hivi sasa serikalini watajiuzulu, lakini badala yake wasichukuliwe hatua ya kufikishwa mahakamani. Mwanzoni, sharti hilo lilipingwa vikali na wapinzani, lakini yaonekana kuwa msimamo huo umebadilika baada ya hadi waandamanaji 130 kuuawa katika miji mbali mbali nchini humo.

Rais Saleh angátuke moja kwa moja

Anti-government protestors shout slogans during a demonstration demanding the resignation of of Yemeni President Ali Abdullah Saleh, in Sanaa, Yemen, Saturday, April 23, 2011. A sea of hundreds of thousands of anti-government protesters swelled along a five-lane boulevard reaching across Yemen's capital Friday in the largest of two months of demonstrations, as the government tried to halt military defections by arresting dozens of officers. Arabic reads on the banner top left, " Ali, you missed the train". (AP Photo/Muhammed Muheisen)
Wapinzani wa serikali wakiandamana SanaaPicha: AP

Duru za upinzani zimesema kuwa pendekezo la wapatanishi kutoka nchi za Ghuba, GCC, linaweza kukubaliwa, lakini kwa masharti. Msemaji wa vuguvugu la upinzani, Mohammed Qahtan, amesema, na hapa ninamnukuu "Kwanza kabisa Rais Saleh ajiuzulu ili serikali mpya ipate kuundwa, ikiwa na rais mpya." mwisho wa kumnukuu. Kwa upande mwingine, msemaji wa vuguvugu la vijana, Khaled al Ansi, amelipinga kabisa pendekezo la GCC. Amesema, wao wanapinga mpango wo wote ule ambao hautopelekea kungoka madarakani hapo hapo Rais Saleh, wanae na jamaa zake.

Kwa maneno mengine, Saleh asiondoke madarakani baada ya siku 30, bali ang'atuke moja kwa moja. Na wapinzani wameonya kuwa tangazo la Rais Saleh kuwa tayari kuondoka madarakani haimaanishi kuwa maandamano ya upinzani yatamalizika. Maelfu ya watu wamekuwa wakimiminika barabarani kudai mageuzi katika nchi iliyo masikini kabisa katika ulimwengu wa Kiarabu.

Mwandishi: Steffe,Peter/P.Martin

Mhariri:Miraji Othman