1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMADI:Taarifa zatatanisha juu ya mripuko wa Ramadi

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCO0

Taarifa za kutatanisha zimetolewa kuhusu mripuko kwenye mji wa Ramadi nchini Iraq.

Jeshi la Marekani linasema mripuko huo uliotokea karibu na uwanja wa mpira mjini Ramadi ni watu 30 waliojeruhiwa kidogo wakiwemo watoto tisa.Lakini kwa upande wa maafisa wa Iraq mripuko huo umesababisha vifo vya watu 18 wengi wakiwa ni watoto.

Hata hivyo haikujulikana mara moja ikiwa taarifa hizo za kutatanisha zinazungumzia tukio moja au kumetokeo mripuko mwingine tofauti.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya kigeni wa Iraq amesema maafisa kutoka mataifa ya eneo hilo zikiwemo Iran na Syria wataungana na wajumbe wa Marekani na Uingereza katika mkutano utakaofanyika mwezi ujao kwa ajili ya kutafuta njia za kuleta usalama nchini Iraq.