1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah. Mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa yavunjika.

5 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5w

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema kuwa mazungumzo na kundi la Hamas yenye lengo la kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na chama chake cha Fatah yamekufa na kwamba anaweza kuivunja serikali inayoongozwa na chama cha Hamas.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice, Abbas amesema kuwa iwapo makubaliano hayatafikiwa hivi karibuni, chochote kinaweza kutokea.

Rice amewaambia waandishi wa habari kuwa Marekani itaongeza juhudi zake kuimarisha hali ya Wapalestina na kuibana Israel kulegeza hatua yake ya kuufunga mpaka wake na Gaza.

Rice baadaye alikutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert, ambaye amenukuliwa na maafisa wake akimueleza Rice kuwa nchi hiyo inamipango ya kufungua eneo muhimu la kibiashara na Gaza hivi karibuni.