1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH:Shangwe zatawala Ukanda wa Gaza

20 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgl

Kundi la kwanza la wafungwa wa kipalestina waliyochiwa na Israel limewasili katika mji wa Ramallah na kupokewa na mamia ya watu waliyowaita mashujaa wa uhuru.

Israel imetangaza kuwaachia wafungwa 256 ikiwa ni sehemu ya kumpa nguvu na umaarufu zaidi Rais wa mamlaka ya wapalestina Mahamoud Abbas wa chama cha Fatah anayeungwa mkono na Marekani.Pia hatua hiyo ni katika juhudi za kukitenga chama hasimu cha Abbas chama cha Hamas.

Wengi wa wafungwa waliyoachiwa ni wale wanaotoka katika chama cha Fatah wakiwemo wanawake sita pamoja na Abdel Rahim Malouh ambaye ni kamanda msaidizi wa tawi dogo la kijeshi la Fatah, Popular Front for the Liberation of Palestina PLO.

Wakati huo huo mkuu wa siasa za nje wa umoja wa Ulaya Javier Solana yuko Mashariki ya Kati katika juhudi za kufufua mazungumzo ya amani kati ya Israel na wapalestina.