1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANAA: Al Qaida yauwa watalii saba wa kihispania

3 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmB

Watalii saba wa Uhispania na raia wawili wa Yemen wameuawa katika shambulizi la kigaidi la kujitoa mhanga huko Yemen.

Wizara ya mambo ya nje ya Uhispania imesema kuwa watu wengine sita walijeruhiwa katika shambulizi.

Rais Ali Abullahi Salehe wa Yemen amesema kuwa mamlaka za kiusalama nchini humo zilifahamu njama za Al Qaida kushambulia maeneo ya nchi hiyo.

Hata hivyo amesema kuwa mbali ya hatua za kudhibiti usalama kuchukuliwa katika maeneo ya serikali visima vya mafuta lakini hekalu la Balqis linalotembelewa na watalii halikutiliwa uzito

Mtu wa kujitoa mhanga akiwa na gari lililosheheni milipuko alijibamiza katika msafara wa watalii hao wa kihispania huko katika mji wa Marib kiasi cha kilomita 150 kaskazini mwa mji mkuu wa Yemen Sanaa.

Serikali ya Uhispania imetuma ndege yenye madaktari na madawa kwa ajili kuchukua miili ya wahanga hao na majeruhi